Friday, 23 October 2015

PERSONAL SELF-AWARENESS  (KUJITAMBUA BINAFSI)

Kujitambua ni jambo la muhimu sana katika maisha ya kila mwanadamu kumuwezesha kufikia mafanikio katika nyanja zote.Faida za kujitambua Mtu anayejitambua: 1. Anaweza kuishi na watu wa aina mbalimbali kwa amani na furaha 2. Anaishi maisha yasiyo na majuto 3. Hawezi kumlaumu Mungu 4. Anayasimamia maono yake vilivyo na kujiamini 5. Anaweza kufanya mambo makubwa 6. Hapati shida kwenye mahusianoKUNA MAMBO MANNE (4)UNAPASWA KUYAANGALIA ILI UWEZE KUJITAMBUA KIKAMILIFU KWA KIFUPI TUNAVIITA  UMAFUTIUsifuate mkumbo jitambue kwanza kwa kujiuliza maswali yafuatayo:

a)  Mimi ni nani?
b)  Nimezaliwa au Nimeumbwa na Mungu kwa makusudi gani?
c)  Nina nini?
d)  Ninatoka wapi na ninaelekea wapi?

KIPIMO CHA KUJITAMBUA NI UMAFUTI

a)   UWEZO
  • Ni pamoja na 
  • Afya yako,
  • Elimu yako
  • Uchumi uliyonao,
  • Vipaji,
  • Marafiki…..

b)  MAPUNGUFU
  • Tabia mbaya uliyonayo ,
  • Kufuata mkumbo
  • Kutokujiamini
  • Ukosefu wa kuwa mbunifu,
  • kushindwa kufanya maamuzi sahihi,
  • kukurupuka,
  • kutokupenda ushirikiano na wengine ….

c)    FURSA
  • Mahali ulipo,
  • Rasilimali watu waliokuzunguka(Ndugu ,jamaa na marafiki ) ,
  • Vipaji ulivyo navyo,
  • Fedha unazopata
  • Mungu

d)    TISHIO
  • Ushindani kila kona mfano katika mahusiano,elimu,ajira,biashara,Ibilisi mwenyewe hapendi ufanikiwe.
  • Maadui zako ni wengi .
      • HITIMISHO: Kwa hiyo usijisahau kumbuka kwamba mungu ndiye chanzo cha kila jambo jema hata maadui wakikujia Mungu akiwa upande wako hawawezi kufanikiwa hata kidogo.Basi mtangulize yeye kwa kwenda msikitini au kanisani bila ya kuvutwa na mtu yeyote. “Nje ya Mungu hakuna mafanikio yenye faida .”                                                                                                                                             SOMO HILI LIMEANDALIWA NA SAID JAMES 0717 820 980

No comments:

Post a Comment